About Me

+25552505047
Tuijuekweli@gmail.com

IMANI


                                               SOMO LINATOKA KATIKA EFE. 4: 5
1.       Neno imani maana yake (Ebr. 11:1)… Umuhimu wa imani unadhhirika tunaposoma Ebr 11: 6.
Biblia inatufundisha waziwazi kwamba kuna imani moja tu inayokubalika kwa Mungu. (Efe 4:5). Kutokana na ukweli huo mtu anapouliza swali “wewe ni wa imani gani? Katika ulimwengu wa roho anaonyesha kukosa ufahamu wa neno la Mungu. Hakuna mahali popote katika Biblia katika vipindi mbalimbali kuwa zipo imani  nyingi katika kumwelekea Mungu. Madhehebu mbalimbali duniani yanaongozwa na imani nyingi tofauti tofauti lakini machoni pa Mungu kuna imani moja tu na anataka watu wote tufikie umoja wa imani hiyo (Efe. 4: 13) na kuendelea katika imani hiyo. (Mdo. 14: 22)
2.       Je, imani hiyo moja inapatikanaje?
Imani hiyo moja inapatikana kwa kusikia neno la Kristo, (Rum. 10: 17). Dini mbalimbali na hata madhehebu mengi ya Kikristo hutofautiana imani kutokana na kusikia kutoka katika vyanzo vinavyotofautiana. Kwa mfano Yesu alisema Mt. 15: 1 – 3, 8 – 9 na mtume Paulo akisisitiza hayo akisema Kor. 2: 16 – 17 kwa kuwa kuna Injili moja tu iliyo ya kweli kwa hiyo lazima iwepo imani moja ya kweli. Gal. 1: 6 – 9. Roho Mtakatifu anaonya katika Yoh. 1 Yoh. 4: 1. Tena Wakristo tunahimizwa kusimama imara katika imani 1 Kor. 16: 13. Tunatakiwa kuhubiri, kuamini na kutii Injili ambayo ilitolewa mara moja tu. Yud. 3.
Imani hiyo  moja haitakiwi kuongeza au kupunguza chanzo chake yaani mafundisho ya Yesu katika Agano Jipya. Ufu. 22: 18, 19. Shetani anajua kwamba tukiacha imani hiyo, tutakuwa mali yake. Mdo. 13: 8. Tusikubali kupotoshwa kwa ajili ya usalama wa roho zetu.

HASARA YA KUJENGWA KATIKA IMANI ISIYOTOKANA NA MAFUNDISHO YA YESU (Rum. 10: 17)
1.       Kumkataa Yesu kuwa mchungaji mkuu na hivyo kukosa kuwepo katika kundi lake ambalo ni kanisa lake. Yn. 10: 16…………
2.       Kuleta matengano, fitina au faraka tofauti tofauti kabisa na kusudi la Mungu. Yn. 17:  20 – 23. Kwa nini ulimwengu wa leo unapuuza maombi hayo ya Yesu? Jibu sahihi tunalipata Rum.16: 17 – 18
3.       Kukataa mafundisho ya Yesu kunatuletea laana. Gal 1: 6 – 9.  Ni laana aliyoitangaza Mungu hata wakati wa Agano la Kale. Yer. 17: 5…..
4.       Kukataa kujenga imani yako katika msingi wa mafundisho ya Yesu maana yake unaruhuru nafsi yako kufanyika mateka na hivyo kukosa uhuru ulio katika Kristo Yesu. Kol. 2: 8
5.       Kukataa mafundisho ya Yesu au kutumia isivyo halali neno la Mungu, kunasababisha imani ya kweli kutukanwa. 2 Pet. 2: 1 – 3….. (2 Tim 2: 15).
6.       Kukataa mafundisho ya Yesu na kugeukia mafundisho mengine, kunawafanya watu wenye juhudi ya kumtafuta Mungu kwa  nia njema kabisa, kupata hasara ya roho zao katika siku ya mwisho. Rum 10: 1 – 4 kwa kumalizia somo letu la leo hebu turejee maneno ya Yesu. Yn. 14:6
7.       Somo hili lilirushwa hewani PPR tarehe 4/02/2018 (saa 1 – 2 usiku)




Chapisha Maoni

1 Maoni

  1. Halleluya!! Sifa apewe Bwana!
    Aaanteni sana kwa kazi hii kubwa na nzuri. Huu ni mwanzo mzuri sana tena sana.

    JibuFuta